Skip to content

Kolonia Santita: Laana YA Panthera Tigrisi
Stock Photo: Cover May Be Different

Kolonia Santita: Laana YA Panthera Tigrisi Paperback - 2012

by Enock Maregesi


From the publisher

'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi - na duniani kwa jumla.
Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda - na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili - na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.

Details

  • Title Kolonia Santita: Laana YA Panthera Tigrisi
  • Author Enock Maregesi
  • Binding Paperback
  • Pages 406
  • Volumes 1
  • Language SWA
  • Publisher Authorhouse UK
  • Date 2012-09-12
  • ISBN 9781477222959 / 1477222952
  • Weight 1.31 lbs (0.59 kg)
  • Dimensions 9 x 6 x 0.9 in (22.86 x 15.24 x 2.29 cm)
  • Dewey Decimal Code FIC